23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

RAILA, KALONZO KUSHTAKIWA?

NAIROBI, KENYA

MASHTAKA mapya yamewasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Keriako Tobiko, ya kutaka vigogo wa NASA, Raila Odinga na mgombea wake mwenza, Kalonzo Musyoka, kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ombi hilo limewasilishwa na Samwel Waweru Gikuru, kupitia kwa wakili wake, Harrison Kinyanjui. Waweru amedai kwamba, wawili hao wamevunja sheria kwa kusema kwamba hakutakuwa na uchaguzi hapo ifikapo Oktoba 26, mwaka huu.

Gikuru amedai kwamba, Odinga na Kalonzo hawana mamlaka ya kuamua siku ya kuandaa uchaguzi na huo ni uvunjaji wa sheria.

“Matamshi haya yanakusudia kuizuia Tume ya IEBC kuandaa uchaguzi,’’ Gikuru alidai.

Raila na Kalonzo walisema kwamba, hawatairuhusu Tume ya IEBC kuandaa marudio ya uchaguzi kabla ya kuwaondoa baadhi ya maofisa wa IEBC ambao walihusika katika udanganyifu kwenye uchaguzi wa Agosti 8.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles