27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Pistorius afungwa jela miaka sita

Oscar Pistorius
Oscar Pistorius

PRITORIA, AFRIKA KUSINI

BINGWA wa mbio za Olimpiki kutoka nchini Afrika Kusini mlemavu, Oscar Pistorius, amehukumiwa kwenda jela miaka sita kwa kumuua mpenzi wake mwaka 2013.

Mwanariadha huyo awali alitakiwa kwenda jela zaidi ya miaka 15, lakini upande wa mshtakiwa ulipambana na kukata rufaa kwa madai kwamba aliua bila ya kukusudia, hivyo alifungwa kifungo cha nje huku upelelezi ukiendelea.

Hata hivyo, mwanariadha huyo tayari ametumikia kifungo cha takribani miezi tisa jela tangu alipohukumiwa, lakini kwa sasa kifungo chake kimeongezeka baada ya upande wa Serikali kushinda rufaa hiyo ambapo kosa lake lilibadilika na kuwa kosa la kuua kwa kukusudia.

Mwezi uliopita, Pistorius alifikishwa mahakamani kwa ajili ya shauri hilo ambapo wanasheria wake walimtaka kuvua miguu yake ya bandia na kutembea mbele ya mahakama.

Hatua hiyo ya kuvua miguu ya bandia iliyomfanya ashindwe kusimama vizuri ilikuwa na lengo la kumshawishi jaji ili auone udhaifu wake na aweze kumhukumu kutumikia jela kwa muda wote au kumpunguzia.

Hata hivyo, upande wa mashtaka ulitoa hoja na kusema ulemavu wa mwanariadha huyo si jambo la msingi hivyo sheria zifuate mkondo wake bila ya kujali nani amefanya kosa hilo.

Japokuwa adhabu ya kosa la mauaji ya kukusudia nchini Afrika Kusini ni kifungo kisichopungua miaka 15 jela, lakini Jaji Thokozile Masipa, amepindisha kidogo sheria hiyo na kuangalia hisia za mlemavu huyo alivyoonekana kujutia kosa lake.

Wanaompinga mlemavu huyo wameshangaa maamuzi ya mahakama na wamedai kitendo hicho cha kumhukumu miaka sita jela ni udhaifu wa hukumu na ni matusi kwa mahakama pamoja na familia ya marehemu Reeva Steenkap.

Pistorius mwenye umri wa miaka 29, alimfyatulia risasi mara nne mpenzi wake, Reeva alipokuwa anatoka chooni siku ya sikukuu ya wapendanao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles