24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yenye mabadiliko kuivaa Medeama

YANGANA ADAM MKWEPU,DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans van Pluijm, amesema kikosi chake kitakuwa na mabadiliko makubwa katika mchezo wao dhidi ya Medeama ya Ghana, unaotarajiwa kuchezwa Julai 16 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ikilinganishwa na michezo miwili iliyopita ambayo kikosi chake kilipoteza.

Yanga tayari imepoteza michezo miwili muhimu katika hatua hii ya makundi, mchezo wa  ugenini waliocheza dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambao walikubali kufungwa bao 1-0 na mchezo waliocheza nyumbani dhidi ya  TP Mazembe ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) bao 1-0.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema kwamba wamejipanga kutumia akili, mbinu na nguvu ili kupata ushindi wa uhakika na kusonga mbele, hasa ukizingatia safu yake ya ushambuliaji ipo katika wakati mzuri, baada ya kumaliza tofauti zilizojitokeza kabla ya mchezo dhidi ya TP Mazembe.

“Mashabiki wanatarajia ushindi katika mchezo huo, viongozi na wachezaji wenyewe kwa maana hiyo hautakuwa mchezo wa kawaida, ni kati ya michezo minne muhimu katika Kundi A ambao tunatakiwa tushinde ili kuweza kuwa na matumaini ya kusonga mbele,” alisema Pluijm.

Wakati huo huo, Yanga haitaweza kumtumia mchezaji wake tegemeo, Deus Kaseke, katika mchezo huo kwakuwa bado ana majeraha kutokana na ajali ya pikipili aliyoipata eneo la Ubungo, Dar es Salaam wakati akielekea maYNzoezini Uwanja wa Boko Veterani, akitokea nyumbani kwake Kigogo.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema Kaseke atalazimika kuikosa mechi hiyo muhimu baada ya daktari wa timu hiyo, Edward Bavu, kushauri akae benchi kwa muda wa wiki mbili.

 

 

 

Katika hatua nyingine, Salehe alisema kiungo mpya Mzambia, Obrey Chirwa, ambaye alikwenda kwao kwa ruhusa maalumu, tayari amerejea nchini na leo atajiunga na wenzake kujiandaa na mechi hiyo dhidi ya Medeama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles