25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

NASSARI: MADIWANI WA CHADEMA ARUSHA WAMENUNULIWA

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), amesema ana ushahidi wa kununuliwa kwa baadhi ya madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kununuliwa na wateule wa Rais mkoani Arusha.

Aidha, amemuomba Rais John Magufuli kumuonyesha ushahidi huo endapo atahitaji kwani amekuwa akijipambanua kupambana na rushwa wakati wateule wake wanafanya bila kificho katika ofisi za umma.

“Hakuna Diwani wa Chadema aliyehama kumuunga mkono Rais Magufuli, wanaunga mkono rushwa, wanamsingizia rais kwamba wanamuunga mkono kumbe wanaunga mkono rushwa kupitia wateule wake.

“Ninao ushahidi kama rais atakuwa tayari niko tayari kumwonyesha, tuliona kwenye makinikia kwamba anayo hata ‘flash’ na mimi ninayo flash, nitamwonyesha endapo ataridhia,” Joshua Nassari

“Tulikuwa tunajua kinachokwenda kutokea jana tulijua watapokelewa madiwani wawili wa Arusha, tunajua biashara inayoendelea katika ofisi za umma, rais atakapohitaji niko tayari kukutana naye, niko tayari kukutana na Inspekta wa Polisi, Simon Sirro, Mkurugenzi wa Taaisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa,” amesema Nassari.

Pamoja na mambo mengine, Nassari amesema endapo ushahidi wake utakuwa si kweli kuthibitisha madiwani hao hawajanunuliwa kwa rushwa yuko tayari kujiuzulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles