25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MWEKEZAJI TANZANITE ONE AKALIA KAA LA MOTO

Na MASYAGA MATINYI -MANYARA


WAKATI Serikali ya Rais Dk. John Magufuli ikiapa kupambana na wawekezaji wanaohujumu nchi katika sekta ya madini, imebainika leseni inayomilikiwa na Kampuni ya Tanzanite One kwa ubia na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) ni batili.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini ubatili wa leseni hiyo, Mining Licence (ML) 490/2013, unatokana na kukiukwa kwa Sheria ya Madini ya 2010 pamoja na kanuni zake.

Pia imebainika wakati Tanzanite One wakiomba leseni hiyo, waliomba pamoja na kampuni inayoitwa Furahia Madini Company Limited, lakini kinyume chake leseni ilipotoka iliitaja Stamico kuwa mbia.

Leseni hiyo ilitolewa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Juni 20, 2013.

Pia leseni hiyo ilichanganya kundi la madini ya vito na madini ya viwandani kinyume cha matakwa ya Sheria ya Madini ya 2010, ambayo inakataza leseni moja kutolewa kwa uchimbaji wa aina tofauti za madini.

Lakini leseni ya Tanzanite One kwa ubia na Stamico, inaonyesha wanaruhusiwa kuchimba madini aina ya Graphite, Marble na Tanzanite.

Mbali na kuchanganya madini ya vito na madini ya viwandani, pia leseni ina eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 7.6, kinyume na kifungu cha 5 (1) (f) cha Kanuni za Madini za 2010.

Kifungu hicho kinaelekeza leseni ya eneo la madini ya vito kuwa na ukubwa usiozidi kilometa 1 ya mraba au hekta 100.

Katika uchunguzi wake, MTANZANIA Jumapili  limebaini kuwa ….

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles