23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mpinzani wa Putin aachiwa huru baada ya siku 30 jela

MOSCOW, URUSI

MKOSOAJI wa serikali ya Urusi, Alexei Navalny ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku 30 jela kwa kupanga maandamano ya upinzani.

Maandamano hayo yamegeuka kuwa vuguvugu ambalo limeitikisa serikali ya Urusi tangu mwezi uliopita.

Polisi walikuwa nje ya gereza wakati akiachiwa huru lakini hawakuchukua hatua yoyote ya kumkamata tena, kama walivyofanya wakati viongozi wengine wa upinzani walipoachiwa huru hivi karibuni.

Baada ya kuachiwa Navalny ameendelea kuwataka wafuasi wake kuingia mitaani, hatua ambayo inaweza kuwafanya polisi wamkamate tena.

Mara baada ya kutoka jela, kiongozi huyo wa upinzani na mwanarakati wa kupinga rushwa mara moja alilaani kile alichosema kuwa ni vitendo vya kigaidi vilivyofanywa na serikali ya Urusi katika kuyazima maandamano mjini Moscow katika wiki za hivi karibuni.

Awali, Navalny kabla hajapona sasa aliugua ghafla akiwa gerezani.

Ghafla ngozi yake ilianza kututumka na kutoka vipele vidogo vidogo vyekundu hali iliyojenga hofu kwa wafuasi wake kwamba huenda alikuwa amepewa sumu.

Hata hivyo madaktari waliomtibu walisema alipata mzio wa ghafla wakati alipoingia tu gerezani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles