25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MIMI MARS AFURAHIA JUX,VANESSA KUWA PAMOJA

NA CHRISTOPHER MSEKENA


MSANII wa Bongo Fleva na mdogo wa mwanamuziki Vanessa Mdee, Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ amesema anafurahi kuona Jux na dada yake wamemaliza tofauti zao na wamekuwa pamoja tena kama zamani.

Jux na Vanessa Mdee mwezi Mei mwaka huu walitangaza kuvunjika kwa penzi lao kutokana na sababu ambazo kila mmoja hakutaka kuziweka wazi hivi karibuni wameonekana tena pamoja huku wakikonga nyoyo za mashabiki wao kwenye tamasha la Fiesta ambapo wengi wameonyesha kupenda kuwaona pamoja.

Akizungumzia ugomvi wa Vanessa na Jux, Mimi Mars alisema alikuwa anajisikia vibaya kuona wawili hao hawapo tena pamoja kutokana na kuzoea kuwaona wakiwa wote.

“Mimi nafurahi kuona Jux na Vanessa wamemaliza tofauti zao na wanaongea tena kama zamani, ingawa sijui kama wamerudiana kama marafiki tu au kama wapenzi,” alisema Mimi Mars.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles