23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 20 zatolewa kusaidia wanawake wanaougua fistula Lindi

HADIJA OMARY, LINDI

Kampuni ya mafuta na gesi (Equinor Tanzania), imetoa kiasi cha Sh milioni 20 kwa Hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kuwafanyia upasuaji wanawake 80 wanaougua fistula katika Mkoa wa Lindi.

Akitoa salamu za kampuni, Mkurugenzi mkazi wa kampuni hiyo Dk Mette Ottoy amesema  mpango huo  ya matibabu kwa wagongwa wa fistula kwa Mkoa huo utaendeshwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inafanyika mwaka huu na awamu ya pili itaendeshwa mwakani.

Naye Mkurugenzi wa CCBRT Dk Blenda Msangi  amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili akinamama wengi wanaougua fistula katika maeneo yaliyomengi ni kushindwa gharama za matibabu pamoja na gharama za usafiri kutoka maeneo wanayoishi mpaka katika vituo vya kutolea huduma, hivyo wanawake wengi hukosa kupatiwa matibabu ya haraka kwa kushindwa kumudu gharama hizo.

“Takwimu zinaonyesha zaidi wanawake 3,000  wa kitanzania wanapata tatizo la Fistula kila mwaka  hali ambayo huwaacha akina mama hawa katia mazingira magumu  huku mkojo na kinyesi vikiwa vinawatoka bila udhibiti  lakini ni wanawake wachache ambao wanaenda kupatiwa matibabu,” amesema.

“Changamoto nyingine ni imani potofu  ambapo wanawake wengi hudhani ugonjwa wa kutokwa na mkojo ama kinyesi bila udhibiti ni kunatokana na mama wakati wa ujauzito wake kushiriki kimapenzi na wanaume wengi ama kulogwa jambo hilo huwafanya akinamama wengi kuchelewa kuwahi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuona aibu,” amesema.

Kwa upande wake kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dk Stellha Kihombo amesema sababu zinazopelekea  mwanamke kupatwa na tatizo la fistula ni kukosa huduma bora ya afya wakati wa kujifungua, ikiwa sambambana na kuchelewa kufika kwa wakati kituo cha Afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles