23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MIAKA  24 YA  LEWIS HAMILTON FORMULA 1

MARTIN MAZUGWA NA MITANDAO


UNAPOTAJA wakali  wa mbio za  magari  yaendayo kasi  langalanga wanaofanya vizuri hivi sasa huwezi kulikosa jina la Lewis Hamilton, aliyezaliwa katika kitongoji cha Stevenage , Hertfordshire, England, Januari 7, 1985.

Hamilton ambaye ni chotara wa kizungu na kiafrika, mama yake, Carmen Larbalestier, ni raia wa England huku baba  yake, Anthony Hamilton, akiwa ni mweusi  ambao walihamia nchini humo mwaka  1950 wakitokea Grenada, katika visiwa vya Carribean,  alikokuwa akifanya kazi  baba yake.

Mkali huyo alivutiwa zaidi na magari mara baada ya baba yake kumnunulia gari ya kuchezea inayotumia remote kuiendesha jambo lililomvutia zaidi nyota  huyo.

Hamilton mara baada ya kuchezea magari na kuonyesha kuvutiwa nayo, baba yake ndipo alipokuwa akimpa nafasi ya kuangalia mashindano mbalimbali ya mchezo huo ambayo yalivutiwa zaidi na uwezo wa bingwa wa zamani Ayrton Senna, raia wa Brazili.

Mara kwa mara mkali huyo, amekuwa akisema hadharani kuwa licha kupenda mashindano ya magari lakini mtu aliyemfanya akaupenda zaidi mchezo huo ni Senna, ambaye alikuwa moto wa kuotea mbali enzi zake.

Dereva huyo alijiingiza katika mbio za magari akiwa na umri wa miaka nane  mwaka  1993,  katika mashindano ya  Rye House Kart Circuit,  ambayo licha ya kuwa  mara yake ya kwanza alifanya vizuri ingawa hakutwaa taji.

Akiwa na umri wa miaka 10 tu alimuomba bosi wa kampuni ya McLaren F1,  Ron Dennis asaini katika kitabu chake na kumwambia, “Habari naitwa Lewis Hamilton.

“Nitashinda taji la British Championship na siku moja nitakuja kufanya kazi katika kampuni yako,” alisema .

Ingawa ilionekana kama mzaha wakati huo kwa bosi huyo wa kampuni ya McLaren, lakini kumbe kinda huyo alidhamiria kutimiza ndoto zake alizojiwekea.

Dennis alisaini katika kitabu cha Hamilton, wakati huo akiwa bado mdogo lakini mwenye kujiamini mara baada ya kusaini katika kitabu cha nyota huyo, akamwambia.

“Nipigie simu mara baada ya miaka  tisa tunaweza kufanya kitu hapo baadae.” Anasema Dennis.

Mara baada ya miaka nane maisha ya Hamilton yalibadilika kwani alisaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya McLaren,  ambayo aliwahi kuongea na bosi wake akiwa na miaka 10.

McLaren walivutiwa kipaji cha hali ya juu cha  na kinda huyo aliyekuwa akichipukia kwa kasi na kutabiriwa kuwa tishio, kutokana na uwezo wake ambao uliwashangaza wengi.

Ilikuwa Januari 2008, ambapo ilikuwa siku ya kipekee kwa  Hamilton na familia yake ambapo mkali huyo alitwaa taji lake la kwanza katika mbio za magari pale aliposhinda katika mashindano ya Brazilian Grand Prix.

Wakati huo alikuwa tayari ameingia mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia kampuni ya Ma McLaren, mkataba uliofika tamati 2012.

Mwaka 2009 haukuwa wa neema kwa Hamilton licha ya kutwaa taji alijikuta akikumbana na adhabu ya penati  katika mashindano ya Australian Grand Prix, mara baada ya kampuni yake kubadili Gear Box kwenye hatua za mwisho kabla ya kuingia katika mashindano.

Hamilton ambaye amepita katika kampuni nyingi kubwa kama vile McLaren na  Renault, hivi sasa yupo katika kampuni ya Mercedes ambayo imemfanya kung’ara vilivyo kutwaa mataji makubwa.

Nyota huyo ambaye hadi sasa ana mataji matano makubwa, alifungua kabati lake mwaka 2008 alipotwaa taji la Brazilian Grand Prix ambalo amelibeba mara tatu 2008,2009 na 2014 alipokuwa kampuni ya Mercedes.

Mataji mengine aliyowahi kutwaa nyota huyo ni pamoja na  United States Grand Prix, Canadian Grand Prix, Mexican Grand Prix ambayo ameyatwaa mwaka huu akiwa katika ubora wa hali ya juu.

Hamilton ambaye hivi sasa ndiye kinara katika madereva bora, huku akiendelea kuwa mwiba kwa hasimu wake Sebastian Vettel ambaye hayupo katika kiwango bora mwaka huu.

Amemaliza mwezi Oktoba kwa kunyakua taji la Mexican Grand Prix, ambalo upande wake ni taji lake la nne kwa mwaka huu, kubeba mfululizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles