25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MFUMO WA TASAF WAPATA SIFA IGUNGA

Na Abdallah Amiri, Igunga

BAADHI ya wanawake Wilayani Igunga mkoani Tabora waishio katika kaya masikini wameushukuru Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa msaada wa fedha wanazopatiwa kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini.

Mkazi wa Kata ya Igunga, Grace Matriga, ambaye ni miongoni mwa akinamama wanaonufaika na mpango huo alisema tangu afanikiwe kuingizwa katika mpango huo fedha ambazo amekuwa akipewa Sh 64,000 zimemsaidia kusomesha watoto wake shule.

“Ninawatoto wanne Amani Gerald anasoma shule ya sekondari  Mwayunge kidato cha nne Emmanuel Gerlad anasoma shule ya sekondari Igunga kidato cha kwanza huku Wilifrida Gerald  na Witnes Gerald wakisoma  chekechea Shule ya Msingi Igunga,” alisema.

Alibainisha kuwa kabla hajaingizwa katika mpango huo wa TASAF alikuwa hana uhakika kama watoto wake wangeweza  kuendelea na masomo lakini hivi sasa anamshukuru Mungu kuwepo kwa TASAF.

“Fedha ninazopata nanaendelea kuzitumia kwa mahitaji ya wanafunzi ikiwamo sare za shule, madaftari sambamba na vitu vingine,” alisema.

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Wilaya ya Igunga, Dina Madeje, amesema hadi sasa wanafunzi 5763 wa shule za msingi na sekondari pamoja na watoto wa chini ya miaka mitano 6,728 wanasoma shule na kupelekwa kliniki kupitia fedha za mfuko huo.

Hata hivyo Madeje aliongeza kuwa zoezi la uhakiki kwa walengwa wa TASAF  ni endelevu na kuongeza kuwa swala la kupeleka watoto shule na kliniki si la hiari bali ni lazima kwa kila mlengwa wa TASAF.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles