MAMA MKAPA: WAZAZI WANACHANGIA KUSHUKA MAADILI YA WATOTO

0
1200

|Elizabeth Joackim, Dar es SalaamMke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa, amesema wazazi wengi wamekuwa chanzo cha kushuka maadili kwa watoto kwa kuwapa uhuru mkubwa wa kutumia vifaa vya kiteknolojia zikiwamo za kisasa za  mkononi.

Mama Mkapa amesema hayo leo Jumamosi Agosti 25, jijini Dar es saalam katika mahafali ya 14 ya Shule ya Msingi Bahari ambapo amewataka wazazi kuwachagulia vitu vya kuangalia vinavyoendana na umri wao.

“Kutokana na kukua kwa utandawazi wazazi wengi wamejikuta wakiwapa watoto uhuru usio na mikapa jambo linalochangia kushuka kwa maadili miongoni mwa watoto.

‘”Siku hizi unaweza kumkuta mtoto mdogo anajua kutumia simu kuliko hata wewe mtu mzima, mitandao yote ya kijamii kama vile Facebook na instagram anaijua kwa hiyo wazazi tuache kuwa chanzo cha watoto wetu kuporomoka kimaadili,” amesema mama Anna.

Pamoja na mambo mengine, katika mahafali hayo mama Anna ametoa maboksi 10 ya vitabu na vifaa mbalimbali vya maabara kwa shule hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here