MAHAKAMA YAWAHUKUMU WANAJESHI KWA UBAKAJI, MAUAJI

0
908

Juba, Sudan Kusini


Mahakama ya kijeshi nchini Sudan Kusini, imewahukumu wanajeshi 10 vifungo vya kati ya miaka saba na maisha kwa tuhuma za kumuua mwandishi wa habari na kuwabaka wafanyakazi waliokuwa wakitoa huduma za kibinadamu nchini humo.

Kutokana na hilo mahakama hiyo imeiamuru serikali ya Sudan Kusini, iwalipe fidia ya dola 4,000/= takribani shilingi milini tisa za kitanzania kwa kila muathirika wa tukio hilo. Na iilipe familia ya mwandishi, John Gatluak, ngombe 51.

Uhalifu huo ulitokea wakati wa shambulizi lililofanywa katika hoteli ya Terrain, kwenye mji mkuu Juba, mwaka 2016.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliwalaumu walinda amani kwa kushindwa kutoa msaada kwa waathiriwa.

Wanajeshi wa Sudan Kusini, wamelaumiwa kwa kuendesha uhalifu tangu yazuke mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 lakini hilo ndilo shambulizi baya zaidi dhidi ya raia wa kigeni.

Hii ndiyo mara ya kwanza wanajeshi kuhukumiwa kuendesha uovu Sudan Kusini, ambalo ni taifa changa zaidi duniani ambalo lilipata uhuru wake mwaka 2011.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here