23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Lugola aagiza kukamatwa wapinzani wanaomtusi Rais

Na MWANDISHI WETU

MOHA-KILOSA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewaagiza makamanda wa polisi nchini washirikiane na wakuu wa mikoa na wilaya kuchunguza na kuwakamata wapinzani wanaomtukana rais pamoja na Serikali kupitia vikao vyao vya ndani vya siasa.

Akizungumza na wananchi wa mjini Kilosa jana katika mkutano wa hadhara,  Lugola  alisema ana taarifa kuna baadhi ya wapinzani ambao wanafanya vikao vyao vya ndani huku wakitukana, kubeza pamoja na kuwachonganisha wananchi na Serikali yao ambayo inaongozwa na Rais Dk. John Magufuli.  

“Mimi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sitakubaliana na kiongozi wa chama chochote kuvunja agizo tulilolitoa nchi nzima kwa kutokuruhusu kufanyika mikutano ya hadhara ya siasa na pia kupitia mikutano ya ndani ambayo inafanyika, ambapo baadhi ya wanasiasa wahuni wanamtukana rais ambaye ndiye kiongozi mkuu wa nchi, mimi sitakubaliana na hilo,” alisema Lugola.

Aliwataka wapinzani kuwa wasikivu kwa kufuata sheria za nchi na pia kutambua kuwa rais wa nchi hii ambaye kipenzi cha wananchi anapewa heshima yake kwa kuiletea maendeleo nchi.

Lugola alisema Rais Magufuli ni kiongozi ambaye kwa muda mfupi ameiletea mabadiliko makubwa nchi na pia mipango mikubwa ya maendeleo inakuja katika uongozi wake.

Lugola alifanya mikutano miwili ya hadhara wilayani Kilosa, ambapo mkutano mmoja ulifanyika mjini Kilosa na mwingine ulifanyika Tarafa ya Kimamba wilayani humo, ambapo alizungumza na wananchi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi wilayani humo kupitia kutoa nafasi kwa wananchi kutoa kero zao.

 “Nimepata malalamiko ya baadhi ya polisi hapa Kilosa kutokutenda haki katika ukamataji wa watuhumiwa, polisi amepewa taarifa ya mtuhumiwa lakini hamkamati, sasa polisi ambaye ametajwa hapa mkutanoni hakumkamata mtuhumiwa huku uthibitisho ukionyesha kabisa mtuhumiwa amekosa na anapaswa kuwepo kituoni, naagiza polisi huyo akamatwe awekwe mahabusu,” alisema Lugola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles