23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

KOEMAN AHOFIA KUFUKUZWA EVERTON

LONDON, ENGLAND

BAADA ya klabu ya Everton kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Lyon kwenye uwanja wa nyumbani katika michuano ya Kombe la Europa, kocha wa klabu hiyo, Ronald Koeman, ameweka wazi kuwa anahofia kufukuzwa kazi.

Katika michezo 12 iliyopita, klabu hiyo ya Everton imefanikiwa kushinda mara mbili na sasa inashika nafasi ya mwisho katika kundi E la Europa, baada ya kufanikiwa kupata pointi moja kati ya michezo mitatu.

Hata hivyo, klabu hiyo ina kibarua kingine kizito dhidi ya Arsenal katika michuano ya Ligi Kuu nchini England kwenye uwanja wa nyumbani wa Goodison Park, Jumapili hii, hivyo kocha huyo amedai kuwa yupo kwenye wakati mgumu wa kibarua chake.

“Ni wazi kwamba kama timu inashindwa kufanya vizuri kwa upande wa matokeo, ni lawama za mwalimu, lakini siku zote maamuzi ya mwisho yanafanywa na bodi ya timu husika na si kocha mwenyewe, ninajiamini na ninajaribu kila wakati kuhakikisha ninafanya vizuri lakini bado.

“Lakini kama uongozi wa timu utaona haukubaliani na mwenendo wangu, wanaweza kuniambia na nikaangalia sehemu nyingine,” alisema Koeman.

Kocha huyo aliwamwagia sifa wapinzani wake kutokana na kiwango walichokionesha kwenye mchezo huo wa juzi na kudai kuwa, walistahili kushinda.

“Ni kweli wapinzani wetu walicheza katika kiwango kizuri, walicheza huku wakionekana kuwa wanatafuta bao na ndiyo maana walifanikiwa kushinda.

“Nadhani ushindi walioupata unatokana na baadhi ya makosa yaliyofanywa na waamuzi wa mchezo huo, kuna makosa mengi sana wameyafanya, wapinzani wetu kuna wakati walikuwa wanajiangusha, lakini hata kadi ya njano hakuwapa.

“Hata hivyo, mwamuzi aliongeza dakika tano wakati tulifanya mabadiliko ya wachezaji jumla ya sita ambapo ingewezekana kuwa tumetumia dakika tatu, kuna wakati wachezaji waligombana ambapo mgogoro huo ulidumu kwa dakika mbili, kulikuwa na wachezaji nane ambao waliumia uwanjani na kupewa matibabu kwa muda, lakini nikashangaa kuona zinaongezwa dakika tano. Si sahihi,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles