Imechapishwa: Mon, Jul 30th, 2018

JOSE MOURINHO AIKATAA MAN UNITED

MICHIGAN, MAREKANI

BAADA ya Manchester United kukubali kichapo cha mabao 4-1 kwenye michuano ya ‘International Champions Cup’ kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi, kocha wa timu hiyo Jose Mourinho amedai angekuwa shabiki hasingeweza kwenda kuiangalia timu hiyo.

Kocha huyo amedai kipigo hicho kimetokana na uongozi kushindwa kutenga fedha kwa ajili ya usajili alioutaka yeye katika kipindi hiki cha majira ya joto, ambapo alitaka asajili wachezaji watano.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Michigan, kulikuwa na watazamaji 101,254, lakini Mourinho amedai mashabiki wa Man United walipoteza fedha zao bure.

“Hali ya hewa ilikuwa vizuri, lakini kama ningekuwa shabiki nisingeweza kwenda kuangalia mchezo huo, nisingeweza kupoteza fedha zangu kwa ajili ya kuangalia timu hiyo.

“Kwa mfano, niliangalia mchezo wa Chelsea dhidi ya Inter Milan kupitia runinga, mchezo ulikuwa wa ushindani bila ya kujali mashabiki kuwa wachache uwanjani.

“Lakini kwenye mchezo wetu mashabiki walionesha jinsi gani wanapenda klabu yao, walijitokeza kwa wingi, lakini walishindwa kupata walichokifuata,” alisema Mourinho.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

JOSE MOURINHO AIKATAA MAN UNITED