23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

IRAN YATOA MASHARTI YA MPANGO WA NYUKLIA

TEHRAN, Iran

SERIKALI ya Iran imesema kuwa inaweza kuachana na mpango wake wa nyuklia endapo Marekani itaacha kutengeneza dhana zinazotumia nishati hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Spika wa Bunge la nchi hiyo, Ali Larijani, alisema kuwa jambo hilo lipo wazi na linawezekana na akasema kwamba hatua zozote zitakazochukuliwa na Marekani kwa kuziwekea vikwazo nchi yao na Russia, kunaweza kusababisha machafuko katika uhusiano wa kimataifa.

“Hakika ni jambo ambalo linawezekana,” alisema Spika huyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu suala hilo.

“Wanaonekana kuwa wameanza harakati fulani ambazo kwa muda si mrefu zitasababisha ukosefu wa amani katika nyanja za kimataifa,” aliongeza spika huyo katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Spika wa Bunge la Russia, Vladimir Volodin.

Alisema uthibitisho wa hayo ni vikwazo  ambavyo wametangaza dhidi ya Iran na  Russia, pamoja na hatua ambazo hivi karibuni Marekani na washirika wake walianza kufanya kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran.

Alisema katika kipindi cha miezi  ya hivi karibuni  Marekani imekuwa ikijaribu kuvuruga makubaliano hayo na akaishukuru ilivyopigana kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje,  Sergei Lavrov, ambaye alihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofanyika hivi karibuni, jijini  New York.

“Katika mkutano huo, Lavrov alisema wazi  na kwa ufasaha kwamba Marekani inavuruga makubalino ya  JCPOA,” aliongeza spika huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles