23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Indonesia yaandaa mafunzo

NA TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM
INDONESIA imeandaa mafunzo ya kilimo kwa maofisa kilimo wa nchi za Afrika na Mashariki ya Kati yanayolenga kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Dar es Salaam jana , Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Diplomasia ya Umma katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Esti Andayani alisema nchi hiyo imeandaa mafunzo yanayofanyika Mei 17 hadi 23 mwaka huu huko Mkindo, mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo yamejikita katika kuzijengea uwezo nchi za Afrika na Mashariki ya Kati katika uzalishaji na uongezaji thamani mazao, alisema.
“Kilimo kinachangia kwa asilimia kubwa katika uchumi wa Indonesia, hivyo tuliamua kuanzisha mradi wa kilimo nje ya nchi ulioko Mkindo Morogoro unaojulikana kama FARTC,” alisema Andayan.
Andayani alisema mafunzo yatahudhuriwa na wataalamu wa kilimo 13, watanzania wakiwa saba, wawili kutoka Msumbiji na mmoja mmoja kwa nchi za Ethiopia, Madagascar, Sudan na Kenya.
Wataalamu watakaohudhuria watajifunza jinsi ya kuvuna na mabaki kutumika tena hali itakayosaidia kuwa na ziada ya chakula.
Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo wa Mafunzo hayo, Profesa Fidelis Myaka alisema Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za kilimo.
“Tatizo linalotukabili ni ukosefu wa maji ya uhakika katika kilimo cha umwagiliaji na kutotumika vizuri teknolojia mpya za kilimo,” alisema Myaka.
Alisema changamoto nyingine ni ukosefu wa raslimali fedha na masoko ya uhakika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles