25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

IJUE NDEGE YA KIFAHARI KULIKO ZOTE DUNIANI

VYOMBO vya usafirishaji majini daima hutoa somo tofauti na vile vya usafiri wa anga hasa linapokuja suala la ufahari na ughali.

Kwamba ndivyo vinavyopiga hatua haraka katika uboreshaji wa huduma na mwonekano wake kianasa kulinganisha na vile vya usafirishaji wa anga.
Lakini kuna matumaini kwa vyombo vya usafirishaji wa anga kupata suluhu ya kuachwa nyuma na vile vya majini.

Ni baada ya kampuni ya usafirishaji ya Marekani, Crystal Skye, kuzindua ndege mpya mwezi uliopita, mbayo inahesabika kuwa ndiyo ndege ya usafirishaji ya kifahari zaidi duniani kwa sasa.

Kama ilivyo kwa boti kubwa za anasa, ndege hii ikiwa angani inaweza kuwavinjarisha abiria angani kwa siku 14, 21 au 28 katika maeneo mbalimbali duniani.

Ndege hiyo ya aina yake aina ya Boeing 777 200LR ina uwezo wa kuchukua abiria 88.

Pamoja na mambo mengine ina viti vinavyoweza kugeuka kitanda, mtandao wenye kasi wa intaneti na eneo la mapumziko.

Kadhalika ina eneo la kulia chakula, vyombo vizuri vya udongo, glasi za aina yake, baa vinavyoifanya kuwa katika mwonekano wa moja ya migahawa ya bei mbaya duniani.

Kwa sababu hiyo, namna eneo hilo la ndani lilivyo, linaifanya kuwa ndege ya kifahari kuliko zote duniani kwa sasa linapokuja suala la ndege za kibiashara za usafirishaji abiria.

Ikiwa imezinduliwa na kampuni ya Marekani ya usafirishaji ya Crystal Cruises mwezi uliopita, tiketi za uzinduzi za kuvinjari nayo kwa wiki mbili zinaanzia dola 50,000 sawa na Sh milioni 120 kwa kichwa.

Licha ya bei hiyo mbaya wakati wa uzinduzi viti vyote tayari vilijaa, kitu ambacho hakishangazi katika dunia hii yenye watu wanaojua kutumia fedha na wasiopenda kupitwa na mambo.

Mbali ya kuwa na eneo la ndani la nyota tano, abiria pia hupewa huduma za hali ya juu wakiwa angani.

Katika eneo la abiria kuna jumla ya viti vya 88 vilivyo staili ya makochi, mbayo inamfanya mteja kufurahia safari yake kuzidi thamani ya fedha aliyotoa.

Kuna mabafu ya aina yake ya kuogea yaliyonakishiwa kwa mitindo mbalimbali ghali ya kiitaliano.

Katika baa yake yenye kila kitu kinachopatikana katika baa za aina hiyo duniani kuna televisheni kubwa, huduma bure za Wi-Fi na usikilizaji muziki wowote ule.

Akizungumza katika uzinduzi wa ndege hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Crystal, Edie Rodriguez, alisema; ‘Crystal Air Cruises si tu ni kitu kipya kwa kampuni yetu bali pia maendeleo ya sekta ya usafirishaji wa anga duniani.

Kampuni hiyo mbali ya utoaji wa huduma za kifahari za usafirishaji abiria kwa njia ya anga pia ina meli za kifahari ambazo matajiri wakubwa duniani huzitumia kuvinjari dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles