HIZI NDIZO KAULI ZILIZOMPONZA ZITTO

0
53

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe anashikiliwa na polisi katika Kituo cha Chang’ombe, jijini Dar es Salaam ambapo anaendelea na mahojiano akituhumiwa kufanya makosa ya uchochezi kupitia kauli zake akiwa katika kampeni za udiwani.

Kwa mujibu wa Kamati ya Sheria na Katiba ya Chama cha ACT-Wazalendo, katika sehemu ya mahojiano hayo, Zitto amedaiwa kuwashawishi wananchi wasiichague Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa sababu serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu hadi siku hiyo.

Pia, amedaiwa kuwashawishi wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach, hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.

Zitto anadaiwa kutoa kauli hizo juzi Oktoba 29, alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke kauli ambazo zimedaiwa na polisi zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani. Mbunge huyo anaendelea na mahojiano kituoni hapo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here