Harusi ya Priyanka, Nick Jonas yatikisa

0
1727

MUMBAI, INDIASTAA wa muziki na filamu nchini India, Priyanka Chopra, jana alifanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake, Nick Jonas, nchini humo huku mastaa mbalimbali wakijitokeza.

Harusi hiyo imetajwa kuwa moja kati ya harusi kubwa zilizoacha historia nchini humo, ambapo sherehe zake zimefanyika kwa siku tatu kabla ya kufungwa kwa harusi hiyo.

Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi kirefu, lakini Julai 18 mwaka huu walivishana pete na kutangaza kufunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu mara baada ya kukamilisha ndoa ya kimila.

Baadhi ya mastaa waliojitokeza kwenye harusi hiyo ni pamoja na Kelly Ripa, Jay Sean, Lily Aldridge, Jonathan Tucker, Nyle DiMarco, Mindy Kaling, Liza Koshy, Julianne Hough, Lilly Singh na Abhishek Bachchan.

Hata hivyo, mastaa waliokosa kuhudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Lily Collins, Kate Hudson, Olivia Culpo, Selena Gomez na Miley Cyrus, lakini wote walituma salamu za pongezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here