28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ghasia zazuka kisiwa cha Anjouan

ANJOUAN, COMORO

WAKAZI wa kisiwa cha Anjouan nchini Comoro wamesema kumekuwa na milio ya risasi katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Mutsamudu, baada ya vikosi vya ulinzi kuvunja vizuizi vya barabarani, serikali inavyosema viliwekwa na upinzani.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Mohamed Daoudou amewalaumu waandamanaji kwa kutumia silaha za moto na kupinga madai kuwa askari wake walifyatua risasi.

Amesema Gavana wa Anjouan Abdou Salami Abdou, ambaye anatokea upinzani ndiye aliyepanga na kusababisha machafuko hayo.

Kumekuwa na maandamano na wandamanaji wengi kukamatwa katika kisiwa hicho chenye mkusanyiko wa visiwa vingi katika Bahari ya Hindi tangu Julai mwaka huu.

Machafuko hayo yanatokana ushindi wa Rais Azali Assoumani katika kura ya maoni yenye utata iliyomaliza utamaduni wa kuongoza kwa mzunguko katika nchi hiyo yenye visiwa vikubwa vitatu.
Ushindi huo unamaanisha kwamba Rais Azali ataendelea kubakia madarakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles