23.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

DC atishia kusitisha huduma vivuko Kigamboni

Norah Damian, Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, ametishia kusitisha huduma za vivuko vya MV Kigamboni na MV Kazi endapo Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) hawataboresha huduma ya usafiri wa majini.

Hatua hiyo inatokana na ziara ya DC huyo ambaye aliambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo, kufanya ukaguzi katika vivuko hivyo leo asubuhi Jumatano Septemba 26 na kubaini kuwapo kwa mapungufu kadhaa.

“Tumebaini mapungufu mengi sana, nimetoa maelekezo kama hayatafanyiwa kazi tutafunga kwa sababu tuna daraja letu la Mwalimu Nyerere tutalitumia.

“Kuna tatizo la usimamizi katika uendeshaji wa vivuko hivi, hakuna kamera za usalama ndani ya vivuko, namba za simu za dharura na abiria kutokuwa na elimu juu ya matumizi sahihi ya vivuko na kujiokoa.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Temesa, Injinia Sylvester Semfukwe, amesema MV Magogoni kina uwezo wa kubeba tani 500 ambazo ni sawa na abiria 2,000 na magari 61 wakati MV Kazi kina uwezo wa kubeba tani 170 ambazo ni sawa na abiria 800 na magari 22.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles