25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu Ruwa’ichi aanza mazoezi

AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

HALI ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Ruwa’ichi, inaendelea kuimarika baada ya kutolewa katika mashine iliyokuwa inamsadia kupumua na kuendelea kufanya mazoezi.

Askofu Ruwa’ichi alifikishwa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili (Moi) akitokea Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu saa tano usiku ambako alifanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo kwa saa tatu.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Moi, Patrick Mvungi aliiambia MTANZANIA jana Dar es Salaam kuwa jopo la wataalamu wa afya saba wanafuatilia hali ya Askofu Ruwa’ichi kila baada ya saa moja.

“Kwa sasa Askofu bado yuko ICU, lakini hatumii mashine ya kusaidia kupumua, hii inaonyesha dalili nzuri na pia wataalamu wameanza kumfanyisha mazoezi ya viungo akiwa kitandani, hivyo watu wasiwe na wasiwasi kwa sababu afya yake inaendelea kuimarika siku hadi siku.

“Baada ya mazoezi ya kitandani ataanza mazoezi ya kutembea na baada ya afya yake kuimarika zaidi  atahamishiwa High Depend Word (HDU). Hii wodi ni maalumu kwa ajili ya wagonjwa ambao afya zao zimeimarika,” alisema Mvungi.

Alisema matokeo bora ya utendaji wa madaktari yanaonekana kwani hadi sasa ufahamu umeshamrudia.

“Akiambiwa kitu na daktari anafuata maelekezo, pia anaweza kuongea, anakula chakula vizuri na anawatambua watu, hii ni dalili njema kwa mtu aliyefanyiwa operesheni ya ubongo,” alieleza Mvungi.

Juzi Daktari Bingwa wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu katika Taasisi ya Moi, Professa Joseph Kahamba, alisema Askofu Ruwa’ichi anasumbuliwa na tatizo la damu kuvuja kwenye ubongo linaloitwa kwa kitaalamu ‘Chronic Subdural Hematoma’.

Hata hivyo, alisema kabla ya kupelekwa Moi, alikuwa tayari ameshaanza kupatiwa matibabu Hospitali ya KCMC hivyo madaktari wa huko waliona kuna uhitaji wa kupata matibabu zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles