25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Asasi yatoa elimu kwa wasichana 4,000

Nyohana Paul, Mwanza

SHIRIKA lisilo la kiserikali la EAHP-TANZANIA ‘Afya ni Mtaji’ limefanikiwa kuwafikia wasichana na vijana zaidi ya 4,000 jijini Mwanza nje na ndani ya shule kwa kuwapatia elimu ya kujitambua na elimu ya afya ya uzazi ili kupiga vita ukatili wa kijinsia.

Hayo yalielezwa juzi jijini Mwanza na Meneja Mradi wa shirika hilo, Cecilia Nyangasi katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawake ambao hadi sasa ndio waathirika wakubwa wa ukatili wa kijinsia nchini.

Nyangasi alisema  katika mradi huo wa ‘Msichana Amka’  unaotekelezwa katika kata nne wilayani Nyamagana na Ilemela jijini hapa, si tu unawalenga vijana na wasichana bali pia watu wazima kwani wanaume na wanawake zaidi 19000 wameweza kufikiwa na elimu hii.

Alisema malengo ya mradi ni kuona ongezeko la wasichana na wanawake vijana wanakuwa na uthubutu wa kushiriki masuala ya kijamii kwa kuwawezesha kupitia huduma za kijamii ikiwemo elimu ya afya, ushauri nasaha na  msaada wa kisheria.

Kwa upande wake Elisiana Temu mwezeshaji kutoka Eahp, alisema ndani ya mwaka mmoja wa mradi wamefanikiwa kuongeza mwamuko ndani ya jamii  kwani kwa kipindi hiki cha siku 16, makundi mbalimbali ya watu wamepatiwa elimu ya uzazi na ukatili wa kijinsia.

“Lengo letu ni kuyafikia  makundi mbalimbali ya vijana hasa watoto wa kike waweze kujitambua  kwa kujua afya ya uzazi ambao ndio tutawafanya kuwa mabalozi wa kupiga vita ukatili wa kijinsia, na mpaka sasa tuliowapatia elimu wengi wao wameweza kuonyesha mfano kwa kuanza na kuwa tayari kupima magonjwa kama vile ukimwi na saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake” alisema Temu.

Alisema “kwa sasa tunaendelea na mpango mkakati wa mafunzo ya waelimishaji rika mwalimu na mwanafunzi ambao watatoa ujumbe wa elimu ya afya ya uzazi kupitia virabu vya afya na michezo kwani tumebaini kuwa kupitia mashule tutaweza kuwafikia wasichana wengi zaidi moja kwa moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles