23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

AKOTHEE ANUSURIKA AJALI MBAYA

NAIROBI, KENYA


MSANII anayetamba nchini Kenya, Esther Akoth, amenusurika ajali mbaya baada ya nati za tairi ya mbele ya gari yake kufunguka huku gari hiyo ikiwa kasi.

Msanii aliungana na meneja wake pamoja na dereva, wakitokea Rongo na kuelekea mjini Nairobi, ghafla msanii huyo alisikia sauti tofauti kwenye tairi na ndipo alipomwambia dereva wake asimamishe gari na kuchunguza.

“Nadhani ingekuwa ajali mbaya, tulikuwa kwenye kasi kubwa nikawa nasikia sauti tofauti kwenye tairi ndipo nikamwambia dereva asimamishe gari ili tulikague, tulikuta baadhi ya nati za tairi ya mbele zimeanza kutoka.

“Nadhani kama ajali hiyo ingetokea basi dereva asingeweza kulimiliki gari hilo, lakini tunashukuru tuliweza kugundua mapema tatizo hilo,” alisema Akothee.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles