25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Natasha: Majina ya Kiingereza kwenye filamu yana mvuto

NatashaMWIGIZAJI wa siku nyingi nchini, Susan Humba ‘Natasha’, amesema wazalishaji wa filamu wengi wa Tanzania walikuwa wakitumia majina ya Kiingereza kwenye filamu zao kwa madai kwamba huvutia yanapotamkwa tofauti na ya Kiswahili.

“Wazalishaji wa filamu hizo walikuwa wakidai kwamba majina hayo huvutia kutamkwa mfano ‘My love’, inavuta na inatamkika vema kuliko ‘Mpenzi wangu’.

Hata hivyo, alieleza kwamba miaka ya sasa wengi wamebadilisha hulka hiyo na kutumia majina ya Kiswahili yenye maana husika wa matukio yaliyopo katika filamu zao na yanafanya vema sokoni.

“Mkiangalia kwa miaka ya sasa mambo hayo yanaonekana kupotea na waandaaji wengi wameelimika wanatumia majina mengi ya Kiswahili na yanaonyesha kufanya vizuri hivyo kuua hulka kwamba majina ya Kiingereza tu ndiyo yenye soko yanapowekwa katika ‘kava’ za filamu za kibongo,” alimaliza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles