23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Ukubwa wa jina la Sarafina haumsumbui mumewe

??????????????????????????MUME wa mwigizaji wa Afrika Kusini aliyewahi kutamba katika filamu ya ‘Sarafina’, Leleti Khumalo ‘Sarafina’, Skhutmazo Khanyile, amesema ukubwa wa jina la mke wake huyo haumpi changamoto yoyote katika ndoa yao.

“Jina la Sarafina ni kubwa mno ndani ya Afrika Kusini na nje lakini nilipomuoa na kukubali kuwa mke wangu amekuwa mke kweli kwa maisha halisi si ya kuigiza, anapokuwa nyumbani huwa mke na akiwa kwenye sanaa huwa Sarafina hakuna changamoto yoyote kwenye ndoa yetu,’’ alieleza Khanyile na kuongeza:

“Kwa sasa tuna watoto wawili tunaoishi nao kwa furaha na amani na Sarafina anaendelea kuigiza kwa ambao hawajamuona katika filamu mbalimbali kuna tamthilia inaonyeshwa na televisheni za huku Afrika Kusini anaendelea kama kawaida na kizuri zaidi ana upendo kwa watu wa rika zote ndiyo kikubwa ninachoamini kitamsaidia kuendeleza sanaa yake ya uigizaji.”

Licha ya kucheza kwa mafanikio filamu ya Sarafina, pia Leleti amecheza filamu nyingi ikiwemo ya ‘Yesterday’ zote zikieleza maisha yalivyo magumu katika nchi zenye vita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles