KOFFI ANNAN KUZIKWA GHANA, ALHAMIS

0
854

Accra, GhanaMwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, ambaye amefariki Agosti 18, umewasili katika nchi aliyozaliwa, Ghana ikiwa takribani siku 27 zimepita tangu kifo chake.

Mwili wake umewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra Ghana ukiwa umesindikizwa na familia yake pamoja na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa.

Anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi ya Septemba 13, 2018 huko nchini Ghana.

Kofi Annan amefariki akiwa na miaka 80 aliugua muda mfupi akiwa nje ya nchi yake aliyozaliwa ya Ghana.
Kofi Annan ameongoza Umoja wa Mataifa kuanzia 1997 hadi 2006 amefanikiwa kushinda tuzo ya amani ya Nobel Peace Prize.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here