31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

ZITTO AACHWA MPWEKE ACT – WAZALENDO

NA TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi wa Chama cha ACT Wazalendo, Samson Mwigamba na wenzake tisa, wamejivua uanachama wa chama hicho na kutangaza kusudio la kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwigamba alisema wamechukua uamuzi huo kutokana na baadhi ya viongozi wa chama hicho kutoka nje ya misingi iliyoasisi chama hicho.

Sababu nyingine ni kutukanwa na baadhi ya wanachama na viongozi kutokana na uamuzi wake wa kujiuzulu wadhifa wake huku viongozi wakuu wa chama hicho wakinyamaza kimya.

“Kwenye majukwaa hayo ambako nimetukanwa viongozi wote wakuu wa chama wapo lakini wameshindwa kuwakemea wanaotukana,” alisema Mwigamba.

Orodha hiyo ya kina Mgamba inakuja baada ya viongozi wengine waanzilishi wa chama hicho kuteuliwa na Rais Magufuli katika nafasi mbalimbali.

Hao ni pamoja na Mshauri wa chama, Profesa Kitila Mkumbo (Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji), Mwenyekiti Anna Mgwira, (Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro), Mshauri wa sheria, Albert Msando aliyejiuzulu kutokana na kashfa za picha mtandaoni.

Mwigamba alisema wamechagua kujiunga na CCM kwa sababu kinaakisi itikadi, falsafa na sera za ACT Wazalendo.

“Sababu nyingine ni kujiunga katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi kama azimio la Tabora katika ukurasa wa 17 na 18 linalozungumzia kuporomoka kwa maadili,” alisema Mwigamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles