25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

World Vision yafunga ufadhili mradi wa maendeleo

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

SHIRIKA la World Vision Tanzania (WVT), limefunga ufadhili wake katika mradi wa maendeleo ya jamii uliopo Tarafa ya Mukulat, Halmashauri ya Arusha, Mkoa wa Arusha.

Mradi huo umekabidhiwa kwa jamii, chini ya usimamizi wa Serikali baada ya kufadhiliwa na WVT ikishirikiana na World Vision Australia kwa miaka 15.

Akizungumza mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Miradi ya World Vision, Johnson Robinson, alisema mradi huo umemaliza muda wa kufanya kazi na jamii ya Kukulat iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

“WVT imemaliza muda wake, lakini Serikali na wadau bado mpo, tunaomba mafanikio yaliyopatikana kupitia mradi huu yalindwe na kudumishwa kwa faida ya watu wa Mukulat na Taifa.

“Kupitia jamii ya Mukulat, tulitekeleza mradi katika kata ya Mwandeti, Musa, Olkokola/Lemanyata, Odonyosambu/Oldonyowasi, Mateves, Kisongo na Oltrumet uliolenga kuboresha maisha ya watoto na familia zao tangu mwaka 2003.

Mradi uliwezesha jamii ya Mukulati ya miaka iliyopita kuwa tofauti na ya leo kiuchumi, kielimu na kiafya na katika hayo, naishukuru Serikali kwa kutoa miongozo na sera zilizojenga mazingira mazuri kwa wafadhili.

“Mradi huu umewezesha kutoa wataalamu katika sekta za kilimo, maji, elimu, mifugo, afya na uchumi na wahusika wanajivunia matunda hayo yaliyochangiwa na ushirikiano waliopata kutoka serikalini,” alisema Robinson.

Kwa upande wake, Ofisa Mradi kutoka World Vision Australia, Steven Dunham, aliitaka jamii ya Mukulat kuchukua fursa waliyopewa na kujiendeleza zaidi.

“Mradi huu umewezesha kuboresha afya ya jamii, kujengea uwezo wakulima, kuongeza mavuno na mapato, kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shule na kuboresha elimu kwa manufaa ya umma.

“Kingine ni kuongeza upatikanaji wa maji safi, kuongeza uwezo kwa kamati za kujitolea kutoa huduma mbalimbali, kulinda na kufanya utetezi wa watoto,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha, Dk. Charles Mahera, akizungumza kwenye hafla hiyo, alisema mwaka 2018, tathmini ya mradi ilifanyika na wafadhili hawakuongeza muda kutokana na kufikiwa malengo tarajiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles