24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Madini kutumia maonyesho ya Sabasaba kutangaza fursa zilizopo

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wizara ya Madini imepanga kutumia maonyesho mbalimbali nchini kutangaza na kuonyesha fursa mbalimbali zilizopo kwenye Sekta ya Madini ikiwemo uchimbaji ili Watanzania na wadau wanufaike na rasilimali hiyo.

Hayo yamebainishwa amezungumza Juni 30, Kamishna wa Madini, Dk. AbdulRahman Mwanga alipotembelea mabanda ya Wizara ya Madini, Taasisi pamoja na wadau wake katika Maonesho ya 47 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

“Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko ameona kuna umuhimu wa kufanya maonesho haya kwa nguvu kubwa sana ili watu waweze kujua hizi fursa zinazopatikana katika Sekta ya Madini,” amesema Dk. Mwanga.

Amesema Sekta ya Madini inamchango mkubwa kwenye upatikanaji wa fedha za kigeni ambapo zaidi ya asilimia 50 ya fedha zote za kigeni zinazopatikana nchini zinachangiwa na mauzo ya madini nje ya nchi.

Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzakwanza, Francis Daudi inayojihusisha na maandalizi ya maonesho ya 47 ya Sabasaba ameipongeza Wizara ya Madini na Taasisi zake pamoja na wadau kwa kupewa kipaumbele katika maonesho hayo na wizara.

Kwa Upande wake, Mkuu Idara wa Mawasiliano na Uhamasishaji kutoka Chemba ya Migodi, Muki Msami amesisitiza ushiriki wa Kampuni kubwa na za kati za uchimbaji kushiriki katika makongamano mbalimbali ya madini ili kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika migodi yao.

Dk. Mwanga ametembelea mabanda ya Taasisi za Wizara ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) pamoja na banda la Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM), Peak Rare Earths, Tanzania Chamber of Mines, Jitegemee Holdings Ltd, Yaya Resources, Mkonya Investment Ltd, Mining Services Ltd ili kujionea shughuli zinazofanywa na kampuni hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles