23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wapanda Mlima 71 kushiriki Kili Challenge 2024 kupambana na VVU na UKIMWI

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Kampeni ya Kil Challenge 2024 yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI imeanza kwa wapanda mlima 71 kuanza safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro. Kati yao, 52 wamepanda kupitia njia ya Mweka na 19 wanazunguka mlima kwa kutumia baiskeli.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mangwala.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mangwala, aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, aliwapongeza washiriki hao kwa mchango wao wa kishujaa katika kufanikisha malengo ya mwitikio dhidi ya VVU na UKIMWI. Mangwana alieleza kuwa kampeni hiyo pia inatoa fursa kwa jamii na wadau kutambua masuala yanayohusu VVU na UKIMWI pamoja na kuoanisha changamoto zilizotambuliwa na serikali.

Katika kipindi cha kampeni, huduma mbalimbali za VVU, UKIMWI, uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukizwa, na uchangiaji wa damu zitatolewa bila malipo kwa wananchi katika milango ya Machame na Mweka. Mangwana aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kuchangia damu.

Mangwana aliwakumbusha wazazi na jamii kwa ujumla kutimiza wajibu wao katika malezi na makuzi ili kurejesha maadili yaliyoporomoka hasa kwa vijana. Alisisitiza kuwa UKIMWI bado upo, hivyo kila mmoja anapaswa kuchukua tahadhari.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela, alishukuru Mkoa wa Kilimanjaro na KINAPA kwa ushirikiano wao katika kufanikisha kampeni ya Kili Challenge kila mwaka. Dk. Kamwela alisema kuwa upandaji wa Mlima Kilimanjaro kupitia kampeni hii sio tu ni ishara ya kujitolea bali pia inaonesha dhati ya serikali na wadau wake katika kupambana na UKIMWI.

Mkurugenzi Mkuu wa Geita Gold Mining Limited (GGML), Duran Archery, alieleza kuwa GGML itaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha lengo la kumaliza UKIMWI ifikapo 2030 linafikiwa. Aliongeza kuwa juhudi za kuchangisha fedha dhidi ya VVU na UKIMWI ni muhimu na zinahitaji ushirikiano wa sekta binafsi na serikali.

Mkurugenzi Mkuu wa Geita Gold Mining Limited (GGML), Duran Archery.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles