27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM: LOWASSA ANAJITISHA KWA KIVULI CHAKE

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umesema Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, yuko  katika majuto makubwa kutokana na uamuzi wake wa kuihama CCM.

Kutokana na hali hiyo, UVCCM imesema kuwa kiongozi huyo kwa sasa yupo katika mawazo hasa baada ya hali ya kisiasa aliyoikuta ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Tamko hilo ya UVCCM limekuja siku chache baada ya Lowassa kuwakaribisha wana-CCM waliokamatwa wakiwemo wale waliokuwa wanatetea nafasi zao kuhamia Ukawa, kwani ni sehemu sahihi na kuna demokrasia ya kweli kuliko iliyopo CCM.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza na makundi ya vijana, wazee wa CCM wa ngazi mbalimbali wilayani Ilala.

Alisema jambo la kusikitisha kumuona Waziri Mkuu huyo wa zamani akiwataka wanachama walioko CCM kujiunga na Chadema wakati yeye mwenyewe yuko mguu ndani mguu nje.

“Lowasa asiudanganye ulimwengu kama bado angali na mvuto wa kisiasa kama alivyokuwa CCM. CCM ndiyo iliompa heshima, umaarufu na kuheshimika kisiasa. Amehama na sasa amebaki kama samaki aliyetolewa nje ya maji,” alisema.

Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema hakuna mwana CCM yeyote anayetengwa, anayebughudhiwa au kunyanyapaliwa kama anavyodai Lowassa kwa lengo la kutaka kujitutumua kisiasa na aonekane yupo yupo.

“CCM ina furaha kubwa kumuona Lowassa akikubali kuuungana na wale waliomtukana, kumwita fisadi, mwizi na mbadhirifu wa mali za umma, sasa akiwafanya ndiyo marafiki. Itakuaje mtu akutukane mchana kisha usiku akusifu na wewe uone fahari,” alisema.

Alisema Lowassa ameshiriki kutenda kosa la kihistoria katika siasa kwa kukubali kukiacha chama alichokitumikia na kujiunga Chadema, huku aiimrubuni mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru naye amfuate na kumpoteza kwenye na ramani ya kisiasa.

Pia aliwataka wana CCM kutobabaika na maneno ya wanasiasa ambao kwa sasa ni dhahiri wanaonekana kutapatapa na kutaka kujitutumua ili waje juu wakati wamemalizika na kufilisika kisiasa.

“Wananchi wote wanajua yaliofanywa na kundi la mafisadi kuiibia nchi rasiliamli za Taifa, kuingia mikataba ya ovyo, kupora mashamba na Ranchi za Taifa, huku wakifahamu uchumi wa nchi ni kina nani waliouvuruga alafu wakajitia kukimbilia upizani,” alisisitiza Shaka.

Katika ziara hiyo, Shaka amekabidhi kadi kwa wanachama 1560 waliojiunga na CCM kutoka Wilaya ya Ilala, alikabidhi Sh milioni 1.5 kuchangia vikundi vya maendeleo vya uzalishaji vya vijana na ujenzi wa tawi Pugu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles