25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

UCHAGUZI DRC WANUKIA

KINSHASA, DRC

JOTO la kisiasa limeendelea kupanda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC, kufuatia Rais Joseph Kabila kuendelea kusalia madarakani wakati tayari muda wake ulimalizika tangu mwishoni mwa mwaka 2016, lakini sasa Tume ya Uchaguzi nchini humo inatarajiwa kutangaza tarehe rasmi ya zoezi hilo.

Hayo yamethibitishwa na Naibu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) ya nchini humo, Norbert Basengezi. Amesema kalenda ya uchaguzi itatangazwa mwishoni mwa juma hili na mkataba wa Desemba 31 mwaka jana utaheshimiwa na kwamba tayari wamekutana na wajumbe wa taasisi inayofuatilia utekelezwaji wa makubaliano ya Desemba 31, mwaka jana, pamoja na wajumbe wa serikali ili kukubaliana tarehe rasmi ya uchaguzi.

Wakati hayo yanajiri, Shirika la kiraia la Synergie des Femmes, linalowakilishwa na Justine Masika Bihamba, limeeleza kwamba, mashirika ya kiraia yanaweza kuwa na uwezo wa kuliongoza taifa baada ya Rais Kabila na kutaka Umoja wa Mataifa kuingilia zaidi masuala ya usalama.

Mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini DR Congo, huku maandamano makubwa yakiendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini humo. Mapema wiki hii, maandamano makubwa ya kumshinikiza Rais Kabila kuandaa uchaguzi mwaka huu yalifanyika katika mji wa Goma, na siku chache baadaye mjini Bukavu mashariki mwa nchi hiyo, huku watu kadhaa wamekamatwa katika maandamano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles