24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Tawa yakabidhi madawati Shule ya Msingi Changarawe

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imetoa msaada wa madawati 60 yenye thamani ya Sh milioni 5 katika Shule ya Msingi Changarawe iliyopo Kata ya Mzumbe wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro.

Akikabidhi madawati hayo Julai 22,2024 kwa niaba ya Kamishna wa TAWA, Kamanda wa Uhifadhi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Sylvester Mushy, alimhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli, kuwa wataendelea kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo na kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli, ameipongeza TAWA kwa ufadhili walioutoa kwa wanafunzi wa wilaya yake

“Naishukuru TAWA kwa uwepo wake katika Wilaya ya Mvomero kama wadau wa uhifadhi, pia tunaishukuru Serikali kwa mipango yake ya kuiwezesha TAWA kifedha kwa sababu imetusaidia wananchi wa Mvomero kupata madawati na kukabiliana na tatizo la wanyamapori wakali na waharibifu,” amesema.

Amesema madawati hayo yatasaidia kuondoa changamoto ya wanafunzi kukaa chini wakati wa masomo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles