23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Shirika la Masista wa Damu Takatifu ya Yesu latoa elimu na huduma bora kwa watoto yatima

Na Safina Sarwatt,Moshi

Watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu kutoka maeneo mbalimbali wamepatiwa huduma bora za elimu na shirika la masista wa Damu Takatifu ya Yesu kama sehemu ya huduma zao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha Upendo-OKAT kilichopo Njia Panda wilaya ya Moshi, Sister Deodora Mtagona, alisema watoto hao wamepatiwa elimu, huduma za kiroho na kimwili, pamoja na ushauri nasaha ili kufikia ndoto zao za maisha.

Sister Mtagona alieleza kuwa chimbuko la kituo hicho ni kutokana na watoto yatima na wale wa mazingira magumu kukosa huduma muhimu kama elimu, afya, na malazi. Kituo hicho kinajiendesha kwa msaada wa wadau mbalimbali, akiwemo mama Rioba Mosha, mhadhiri katika chuo kikuu cha Marekani, ambaye aliguswa na maisha magumu ya watoto yatima alipokuwa ziarani Tanzania mwaka 2020.

Kituo cha Upendo-OKAT kwa sasa kina watoto 26, wakiwemo wavulana 11 na wasichana 15, ambapo wote wanasoma katika shule mbalimbali za binafsi. Sister Mtagona alitoa wito kwa jamii kuonyesha upendo na kuwalea watoto katika mazingira bora bila kuwatelekeza.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya kituo hicho, Antony Semagi, alisema kuwa bodi hiyo imeona umuhimu wa kuwaendeleza watoto hao ili waweze kujitegemea na kufikia malengo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles