32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaweka wazi juu uraia pacha

Ramadhan Hassan,Dodoma

SERIKALI imesema haipo tayari kutumia uraia pacha ila hivi karibuni itaanza kutumia utaratibu wa hadhi maalum ambao utatoa fursa kwa wenye asili ya Tanzania waliopo nje kuchangia nchi yao.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Aprili 18,2024 jijini hapa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika,Balozi Mbarouk Nasoro Mbarouk wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea miaka 60 ya Muungano.

“Ni kweli muda mrefu kumekuwa na vigugumizi lakini kwa maslahi mapana bado haipo tayari lakini Mheshimiwa Rais ameitoa maelekezo watu wote wenye asili ya Tanzania waliopo nje wachangie nchi yao kwa kupewa hadhi maalum.

Amesema hadhi maalum inatoa fursa kubwa katika kuhakikisha wanachangia maendeleo ya nchi.

Naibu Waziri huyo amesema wananchi wengi waliopo nje wamekubaliana na hivi karibuni baada ya kukamilika taratibu za kisheria hadhi maalum itaanza rasmi.

Naibu Waziri huyo amesema mojawapo ya kazi za mabalozi nje ya Tanzania ni kutangaza fursa mbalimbali ikiwemo za uchumi na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.

Amesema mabalozi pia wamekuwa wakitoa fursa kwa makampuni ya kitanzania kushiriki katika mikutano na maonesho ya kibiashara.

Kuhusu utatuzi wa changamoto wanazokutana nazo watanzania katika Nchi ambazo hazina balozi wa Tanzania,Naibu Waziri huyo amesema mabalozi waliopo jirani wamekuwa wakitatua.

“Balozi anaweza l kuwakilisha Nchi zaidi ya mbili kwa kuhakikisha maslahi ya watanzania yanalindwa mfano ilipotokea vita Ukrain kule hatuna ubalozi,lakini ubalozi wa Moscow, Sweden na Ujerumani walihakikisha watanzania wanapata msaada na waliofanya kazi kubwa,”amesema Naibu Waziri huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles