25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Saudi Arabia yazidi kushinikizwa juu ya mwandishi aliyetoweka

WASHINGTON, MAREKANI

SERIKALI ya Marekani imeongeza shinikizo kwa Saudi Arabia ikiitaka usahihi wa taarifa kuhusu kutoweka kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi.

Mwandishi huyo mwenye asili ya Saudia anayeliandikia gazeti la Washington Post la Marekani, alionekana mara ya mwisho akiingia kwenye ubalozi mdogo wa taifa hilo nchini Uturuki Oktoba 2, mwaka huu.

Mkasa huo umesababisha wabunge wa Marekani kutaka viongozi wa Saudi Arabia wachunguzwe.

Rais wa Marekani, Donald Trump ameeleza kutoridhishwa kwake na maelezo ya Saudia, akiahidi kuhakikisha ukweli unapatikana kuhusu kupotea kwa mwandishi huyo.

“Hatuwezi vumilia vitendo kama hivyo kutokea kwa waandishi ama kwa mtu yeyote,” alisema Trump.

Ameongeza kuwa wanahitaji kila kitu kinachohusiana na kutoweka kwa mwandishi huyo.

 

Maneno ya Trump yanalingana na ya Seneta wa Chama cha Republican, Bob Corker aliyeilaumu Saudi Arabia, mshirika wa muda mrefu wa Marekani katika masuala ya usalama katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Seneti ya Uhusiano wa Nje ya Marekani, alieleza wasiwasi wake kuhusu kutoweka kadhia hiyo, ambayo Saudia imekuwa ikidai Khashoggi aliondoka ubalozini humo kabla ya kutoweka.

Lakini maofisa wa Uturuki wanaamini Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi huo mdogo mjini Istanbul ijapokuwa hakuna ushahidi uliotolewa.

Saudi Arabia imezikanusha tuhuma hizo ingawa pia haijatoa ushahidi wowote kuelezea namna Khashoggi alivyotoka na au kutoweka ilihali mchumba wake alikuwa nje ya ubalozi akimsubiri bila mafanikio.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan pia ameongeza shinikizo lake kwa Saudi Arabia kutokana na kutoweka kwa mwandishi huyo.

Aidha Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair alisema kutoweka kwa mwandishi huyo ni mkasa wa kutisha unaokinzana na jitihada za mwana Mfalme wa Saudi Arabia, Mohamed bin Salman za kuleta mabadiliko nchini mwake.

Blair aliwaambia wanahabari jijini London jana kuwa Serikali za Marekani na Uingereza zimeeleza wazi kuwa ni lazima uchunguzi wa kina ufanyike.

Awali juzi baadhi ya vyombo vya habari vya Uturuki vilionesha vipande vya kamera za usalama za CCTV zinazothibisha eneo ambalo linahusika moja kwa moja na upoteaji wake.

Imebainika kuwa maofisa usalama wa Saudia wamekuwa wakiingia na kutoka nchini Uturuki kupitia uwanja wa ndege wa Istanbul.

Kitu kingine kilichooneshwa kwenye picha hizo ni gari jeusi likiwasili eneo hilo la ubalozi na ambalo linadhaniwa kuhusika katika tukio hilo.

Pia utepe mwingine wa picha hizo za video unalionesha kundi jingine la watu wanaodhaniwa ni raia wa Saudia wakiingia uwanja wa ndege wa Istanbul na ambao pia wanaonekana katika baadhi ya hoteli za mjini huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles