25.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Sababu za wanaume kutokuwa waaminifu katika mahusiano -3

Wiki iliyopita tuliona sehemu ya pili ya makala haya yanayozungumzia sababu za wanamume kutokuwa waaminifu. Hapo chini ni sehemu ya mwisho.

Ilipoishia
Kama kunauwezekano wa kubadili tabia na kushuhulikia hayo malalamiko yake ni bora ukafanya hivyo maana kifua- tacho chaweza kuhatarisha mahusiano yen

  1. Mkanganyiko wa matarajio ya mwanaume

Wako wanaume wengi ambao kabla hawajaoa walikuwa na shauku kubwa kwa wake zao, walikuwa na matamanio au matarajio makubwa kwa wake zao. Wengine walioa wake zao kwasababu ya maumbo mazuri na yakuvutia, wengine ni aina ya familia wanawake hao walizotoka, wengine walioa wakitegemea huyu mwanamke ni mcha Mungu sana, au uliwahi kusikia habari zake nzuri kwa watu na ukatamani sana kuwa naye maishani na mara baada ya kuingia kwenye ndoa bahati mbaya yale mambo uliyokuwa unakiu nayo sana na kuyatarajia unakuta sio yalivyo. Wapo ambao nimeongea nao sana, wanasema walipooa lile umbo zuri sana la mke wake alidhania ndio ustadi wa kitandani baadaye akakuta ujuzi wa tendo la ndoa ni mdogo kuliko matarajio ya mwanaume. Wengine baada ya ndoa wamekuja kugundua tabia zilizojificha kwa mke ambazo hawakuzijua awali, wengine wameibua madhaifu kedekede kwa wake zao ambayo mwanzoni hawakuyafikiria. Hii hali ya matarajio ya mwanaume kufukiwa na uhalisia huua kabisa hamasa ya tendo la ndoa na hapo inakuwa rahisi mwanaume kuanza kutafuta mahusiano mengine nje. 

  1. Kutokupevuka

Wapo wanaume kwenye ndoa hususani wenye umri usio mkubwa sana wamekuwa wakiripotiwa kuchepuka mara kwamara kwasababu tu  bado hawajafahamu umuhimu wa ndoa ili kuithamini, wameoa lakini bado fikra zao zinatawaliwa na marafiki, hawawezi kujisimamia wenyewe, mtu anaweza kukaa baa na marafiki hadi usiku sana bila kujali kwamba ana mke na watoto. Huko nje usiku ndipo fursa za uchepukaji huzaliwa. Wapo ambao wamechelewa kupevuka kutokana na aina ya malezi waliyolelewa na wazazi wao “spoilt children”, hawa hushindwa kuiheshimu ndoa na mke hatakama mke alalamike vipi. Kila siku kesi ni kuhusu michepuko, simu imekutwa na picha za ngono za mwanamke, simu ina ujumbe wa mapenzi na vingine vingi vinavyofanana na hivi. Baadhi ya ndoa za wanaume wa hivi zimevunjika mapema kwasababu wake zao walishindwa kustahimili. Kupevuka hakuangalii sana umri, mwanaume anaweza kuwa na umri wa miaka 40 lakini bado haonyeshi kupevuka. Kupevuka ni kukua au kupanuka kwa uwezo wa kufikiri hususani katika kuithamini na kuiheshimu familia, mke  na ndoa kwa ujumla.


  1. Kujifariji kwamba kila mtu anafanya

Wapo wanaume wengi walioonyesha kuchepuka kwasababu tu ndani yao walikuwa wanakosa umaana wa kuwa waaminifu kwasababu wanaona hata wale watu ambao wao waliwaamini kwamba labda wanaweza kutochepuka na wao pia walichepuka, sasa mtu anasema kumbe kila mwanaume anachepuka, basi yanini kujibanabana wakati namimi ninahamu na fursa inaruhusu. Kile kitendo chakuona wanaume wengi wanatabia ya kutokuwa waaminifu kudhoofisha mioyo ya wanaume wengine kwa kujifariji kwamba kumbe hichikitu sio kipya, kila mtu anakijua na anafanya, chakujitahidi tu ni kutokugundulika. Pamoja na hayo wito wangu kwa wanaume wenye fikra hizi ni kwamba, kuwa kwako mwaminifu kwa ndoa yako hakutakiwi kuyumbishwa na tabia za wengine, usimtegemee mtu kukutengenezea misingi ya uaminifu wa ndoa yako, je kama kila mwanaume anampiga mke wake na wewe ndio uanze kumpiga? Kama kila familia inaugomvi, na wewe ndio utafute ugomvi hata kama hakuna mazingira ya ugomvi? La hasha!!

Ifahamike kwamba, haijalishi ni sababu gani imemfanya mwanaume au mwanamke kuchepuka au kukosa uaminifu katika ndoa yake, madhara ya tabia hii yanaweza kuigharimu ndoa yako kwa kiasi kikubwa sana. Madhara yake yanaweza pia yasiishie kwenu ninyi wanandoa tu bali yakawaathiri hata watoto wenu. Wito wangu ni kila mwanandoa kuithamini na kuiheshimu ndoa yake kutoka ndani yamoyo na sio kinafiki

Imeandikwa na; Dr. Chris Mauki 

Social, Relationship and Counseling Psychologist

UDSM

E – [email protected]

0713407182

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles