27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Parimatch yazindua Chomoka na Ndinga msimu huu wa Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Zikiwa zimepita siku chache tokea kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar, Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch Tanzania imewapa wateja wake na wadau wote wa kubeti fursa ya kujishindia gari mpya na ya kisasa, simu janja na bodaboda kutoka katika kampeni yao ya Chomoka na Ndinga.

Akizungumza Dar es Salaam leo Novemba 23, 2022 Afisa Habari wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohammed amesema kuwa Promosheni hiyo ni mahususi kwa wateja wao wote wa Parimatch wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi hki cha Kombe la Dunia.

“Katika kipindi cha kuanzia Novemba 22, hadi Desemba 26, mwaka huu mteja wa Parimatch akifanya bashiri kwenye mchezo wowote basi ataingia moja kwa moja katika droo wa kuwania gari aina ya Urban Cruiser yenye O kilometa kutoka kwenye Showroom ya Toyota Tanzania, Bodaboda aina ya Hero Hunter 125cc na smartphone aina ya Samsung Galaxy A03 Core (Simu janja),” alisema Ismael.

Aidha Ismael aliendelea kwa kusema kuwa: “Kila siku tutakuwa tunatoa simu mbili (2) na washindi watakuwa wanatangazwa kupitia kurasa zetu za kijamii na Zawadi ya Bodaboda itatolewa kwa wiki mara moja siku ya Ijumaa kupitia droo itakayoruka ITV wiki husika.

“Zawadi ya Gari itatolewa mwisho wa mashindano haya tarehe 27 Disemba ambapo droo kubwa ya kutafuta mshindi wa gari itafanyika siku hiyo,” amesema.

Pamoja na hayo, Ismael amefafanua kuwa katika promosheni hiyo sehemu ya michezo ya TVBET, Live Casino, Casino New na michezo ya Virtual haitaruhusiwi kushiriki katika promosheni hiyo.

Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya 100% mpaka Sh 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nasi! Parimatch imekuwepo nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual.

Mbali na soka, Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles