P Diddy, Kourtney Kardashian wanaswa

‘P. Diddy’
‘P. Diddy’
‘P. Diddy’

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Sean Combs ‘P. Diddy’ amenaswa na mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Kourtney Kardashian wakiwa baa wanapiga ulabu.

Picha zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonesha wawili hao wakiwa wamelewa na kukumbatiana, hata hivyo kupitia akaunti ya Instagram, Kourtney ambaye ni mdogo wake Kim Kardashian, aliweka wazi kuwa walikuwa wanamalizia wiki.

“Picha hazina ubaya wowote lakini nashangaa kuona zimeenea sana, siku zote nimekuwa rafiki wa karibu na P.Diddy hasa kutokana na kazi yake ya muziki, kikubwa ilikuwa ni kumalizia wiki,” aliandika Kourtney

Hata hivyo P.Diddy naye alisema kuwa japokuwa alikuwa amelewa lakini kikubwa ambacho walikuwa wanajadili ni masuala ya muziki na si vinginevyo kama watu wanavyodhani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here