25.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Nyambaya azipa mzuka timu za wanawake Dar

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Lameck Nyambaya amezitaka timu tatu zinazowakilisha mkoa huo katika Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kwenda kucheza kwa kujiamini ili kutwaa ubingwa huo.

Timu zitakazowakilisha Dar es Salaam katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika mwezi huu ni Mbagala Queens ambayo ni mabingwa wa Ligi ya Mkoa huo, Kinondoni Queens na Young Stars Queen.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam akikabidhi kombe kwa nahodha wa Mbagala Queens,Dablat Kazaura.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi na kombe kwa mabingwa Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam leo Aprili 14,2024 kwenye Uwanja Karume.

Amesema kuwa kama viongozi wa mkoa huo wapo kuhakikisha timu zao zinafanya vizuri na kila mwaka zawadi za washindi wa ligi ya mkoa wao zitakuwa zikiongezeka.

“Nawahakikishieni kuwa tupo pamoja na nyie lengo ni timu zetu zikafanye vizuri na kurudi na ubingwa, mkifika kule kazi yenu ni kuwapiga mabao na msitishike bali nyie muwatishe wao,” amesema Nyambaya.

Naye Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam, Somoe Ng’itu, amemshukuru mwenyekiti huyo kutokana na mchango wake mkubwa kuhakikisha ligi hiyo imemalizika vizuri na washindi kupata zawadi.

Katika mashindano hayo bingwa ambaye ni Mbagala amepata zawadi ya Sh 500,000, kombe, mpira na medali, mshindi mshindi wa pili Kinondoni Queens Sh 300,000, medali na mpira na mshindi wa tatu Young Stars alipata Sh 200,000, medali na mpira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles