25.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

NDC kuandaa sheria mpya  kuwezesha uwekezaji

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Shirika la Taifa la Maendeleo(NDC ), limesema linaandaa sheria  mpya ambayo itazingatia hali halisi  ya mfumo wa uendeshaji  uchumi nchini  na kufanya shirika kuwa chombo mahususi  cha serikali cha kuchochea  mabadiliko ya mfumo wa uchumi, biashara, kusaidia maendeleo na kuwezesha uwekezaji.

Akizungumza leo Septemba 26,2023, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji na vipaumbele vya Shirika hilo kwa mwaka wa fedha 2023/24, Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Dk. Nicolaus Shombe amesema  wamekuwa na mchango mkubwa kimapato, ajira   katika pato la taifa.

“Sheria mpya na mfumo wa uendeshaji  wa shirika unaopendekezwa utazingaita haja ya kuweka  mifumo  rahisi  wa kufikia maamuzi  kuliwezesha shirika  kushirikiana na sekta  binafsi na kutumia fursa za kibiashara  zinazojitokeza,”amesema Dk.Shombe.

Amesema mpango mkakati wa shirika  umehusisha na umeainisha maeneo ya mikakati  ambayo shirika linawekeza kwa kushirikiana  na wawekezaji mahiri wa ndani  na nje ya nchi  lengo ni kuifanya NDC ambalo lina nafasi  kuchangia ujenzi  wa Taifa.

“Kuna maeneo muhimu ambayo sekta binafsi  inasita kuwekeza au  inashindwa kuwekeza kutokana  na sababu  uwezo wa mitaji na Teknolojia  muda mrefu  kupata  manufaa  na sababu  nyingine  za kibiashara shirika linaweza kuwekeza  ili kuvutia wawekezaji wengine, “amesema.

Aidha amesema shirika hilo limeweza kufanya  tafiti  mbalimbali  ikiwemo  mradi wa Liganga na Mchuchuma uliopo Wilaya ya Ludewa Mkoa  wa Njombe kubaini uwepo wa mashapo ya chuma kias cha tani milioni  126  eneo kilomita za mraba 10 na makaa ya mawe tani milioni 426 kwenye eneo kilomita za mraba 30.

Amesema  utekelezaji  wa mradi huo  unatarajia kuchimba chuma tani milioni  2.9 kwa mwaka na kuzalisha  bidhaa za chuma  tani milioni moja kwa mwaka.

“Shirika limefikiwa  kulipa fidia ya jumla shilingi bilioni 15.4 kwa wananchi  wanaoishi mahali mradi unapotekelezwa wa miradi ya Mchuchuma  shilingi bilioni 5 na Liganga  shilingi bilioni 10 ambazo zimetolewa na serikali  hadi kufikia Juni 30, mwaka huu na jumla ya wanufaika 1048 wamelipwa kati ya 1142,”amesema.  

Ameongeza kuwa  upatikanaji  wa leseni za wachimbaji wadogo wa makaa ya mawe  unaruhusu shirika kuanza uchimbaji huo ambapo kampuni tano za wazawa zinatarajia kuanza uchimbaji katika eneo la Mchuchuma  ndani ya mwaka 2023/24.

Dk.Shombe amesema shirika limeendelea na mikakati mbalimbali ya kukifufua na kuboresha  kiwanda cha mikakati cha KMTC kilichopo Hai katika Mkoa wa Kilimanjaro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles