28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mzee Chilo, Kijo, Hashim Kambi ndani ya ‘Homecoming’

Kijo na ChiloNA MWANDISHI WETU

MASTAA wengi wa Bongo Movie wamekutanishwa katika filamu mpya ya ‘Homecoming’, inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni, huku ikilenga kubadilisha soko la mauzo ya filamu za Tanzania.

Baadhi ya mastaa hao walioshiriki katika filamu hiyo ni pamoja na Daniel Kijo, aliyekuwa akitangaza kipindi cha Daladala kinachorushwa na televisheni ya Star TV, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Hashim Kambi, Susan Lewis ‘Natasha’ na Abby Plaatjes, aliyewahi kuwa mmoja wa washiriki wa Big Brother Africa.

Waigizaji wengine walioigiza katika filamu hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Alkemist Media ikieleza madhara ya rushwa ni Alpha Mbwana, Magdalena Munisi, Godliver Gordian na Michael Kauffmann.

Kijo aliigiza nafasi ya mhusika mkuu katika filamu hiyo, ambapo anatumia jina la Abel Mshindi, baba yake mzazi ni mzee Chilo na mjomba wake ni Hashim Kambi.

Filamu inaanza kwa kumuonyesha Kijo akirejea nchini kutokea Marekani alipokuwa akisoma masuala ya fedha, anapofika anaajiriwa katika kazi ya benki, lakini akiwa anaishi kwa mjomba wake huku baba yake akiendelea kuishi kijijini.

Anavyozidi kuizoea kazi yake Kijo alijikuta akiingia katika janga la rushwa kutokana na vishawishi mbalimbali, ikiwemo mahitaji zaidi ya anachokipata, ambayo yalikuwa yakihitajika kuwahudumia baba yake wa kijijini na mwanamke aliyekuwa naye kimapenzi.

Kutokana na changamoto za kimaisha, Kijo alijiingiza katika janga la rushwa ambapo aliishia kifungoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles