27.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongera azidi kuchanua Kenya

280629_heroaNA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Simba anayekipiga kwa mkopo katika kikosi cha KCB ya Kenya, Paul Kiongera, ameendelea kung’ara baada ya kuteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji aliyerejea kwa kishindo (Comeback of the Year Award) Ligi Kuu nchini humo.

Kiongera, ambaye tayari Simba imetangaza kumrejesha kundini ili kukitumikia kikosi chao katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazoendelea Desemba 12, mwaka huu, anawania tuzo hiyo pamoja na nyota wa Nakuru RFC, Lawrence Buyachi.

Straika huyo ameingizwa kwenye kinyang’anyiro hicho kupitia tuzo za Mwanamichezo Bora wa Mwaka (SOYA) zinazotolewa kila mwaka nchini humo.

Kiongera, ambaye ameisaidia timu yake ya KCB kuepuka kushuka daraja, pamoja na kurejea uwanjani akitokea katika majeraha, amefanya mambo makubwa akiwa na kikosi hicho, akifunga mabao 11 ndani ya mechi 17, ikiwamo ‘hat-trick’ dhidi ya Thika United.

Kiongera, ambaye mwaka 2012 aliibuka kuwa mshindi wa pili katika tuzo za Mwanasoka Bora wa Mwaka, anapewa nafasi kubwa kumpiku Buyachi.

Wakati akizidi kung’ara huko kwao Kenya, Simba inamwona kama mchezaji sahihi anayeweza kuiimarisha safu yao ya ushambuliaji, akishirikiana na Mganda Hamis Kiiza na wengineo, wakiwamo wanaotarajiwa kusajiliwa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Mbali ya Kiongera, mchezaji mwingine anayetajwa kuwa njiani kutua Msimbazi ni Mkenya Michael Olunga, anayechezea Gor Mahia ya huko, ambaye ameonyesha uwezo wa hali ya juu katika kucheka na nyavu.

Mshambuliaji huyo aling’ara kupitia michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwaka huu na Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Ethiopia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles