24.3 C
Dar es Salaam
Monday, September 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbarali aipongeza TVLA kwa kutoa elimu ya magonjwa ya wanyama

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, Missana Kwangura, ameipongeza Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea Maonesho ya Sabasaba kuhusu uchunguzi wa magonjwa ya wanyama na uchanjaji wa mifugo ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali.

Kwangura alitoa kauli hiyo Julai 9, 2024, alipotembelea banda la TVLA lililopo Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).

Lengo la ziara yake lilikuwa ni kupata elimu kuhusiana na huduma zinazotolewa na TVLA, ikiwemo uchunguzi wa magonjwa ya wanyama, uzalishaji na usambazaji wa chanjo za mifugo, utafiti wa magonjwa ya wanyama na wadudu waenezao magonjwa hayo pamoja na uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo.

“Mbarali tuna mifugo mingi kwa sasa, ipo zaidi ya laki sita. Wafugaji wengi bado hawajafahamu kwa undani umuhimu wa kuchanja mifugo yao, kuichunguza magonjwa na kuipeleka kwenye majosho. Naomba wataalam wa TVLA waje wasaidiane na wataalam wangu kutoa elimu ili wafugaji wasiendelee kupoteza mifugo yao. Mbarali mifugo ni hazina kubwa,” alisema Kwangura.

Naye, Afisa Utafiti Mifugo wa Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Denis Nyakalinga, alimuahidi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kulifikisha ombi lake kwa uongozi ili liweze kufanyiwa kazi. Nyakalinga alisisitiza kuwa TVLA ipo kwa lengo la kuhakikisha inalinda afya za mifugo nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles