22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

CEFZ yajipanga  kutambulisha mbio  za vikwazo  Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital 

Mwalimu wa kujitolea katika taasisi isiyo ya kiselikali ya Creative Education Foundation Zanzibar (CEFZ), Laura Bjorn amesema kuwa ana mpango wa kuutambulisha mchezo mpya wa mbio za vikwazo ‘Obstacle Sports Adventure Racing’ visiwani humo.

Laura, raia wa Denmark anayeishi Zanzibar ameyasema hayo baada ya kuhudhuria mafunzo ya wakufunzi wa mchezo huo yaliyoandaliwa jijini Dar es Salaam na kampuni ya Scope na kusimamiwa na mkufunzi Nayite Statia kutoka visiwa vya Carribean ambaye anatambuliwa na Bodi ya Kimataifa ya Michezo ya Mbio za Vikwazo (FISO).

Mwanzilishi huyo wa  mbio za ‘Kimbia Bila Shaka Zanzi Half Marathon’ amesema mchezo huo ni wa kipekee na ni maarufu kwa kukuza utalii kutokana na kuchezwa zaidi maeneo yenye vivutio.

Mkufunzi wa mafunzo, Statia Nayibe

“Nitautambulisha mchezo huu kwa vijana wadogo Zanzibar, tayari nina mpango huu kuanzia  kwenye shule ya Msingi na Sekondari ya Steiner Waldorf’ ambazo najitolea.

“Tuna nafasi ya kutosha kuweka vifaa vya mbio za vikwazo kwenye eneo la shamba kwa ajili ya vijana kujifunza na kama tutafanikiwa na kutapata mwitikio mzuri hapo tutakuwa na nafasi nzuri ya kueneza maeneo mengine Zanzibar,” amebainisha.

Laura ameongeza kuwa kuna fursa kubwa ya kukuza mchezo huu wa kuvutia Zanzibar ambao pia unajenga ukakamavu na pia kufungua fursa mpya kwa manufaa ya mchezaji binafsi na taifa.

Washiriki wa mafunzo hayo

“Ninapenda mchezo huu kwa sababu unachezwa maeneo ya wazi ambayo yanakupa changamoto mbalimbali na mbinu tofauti kwa kila kikwazo,” amesisitiza.

Amesema matumaini yake siku zijazo Zanzibar inaweza kutoa wachezaji nyota wa mchezo huo watakao wakilisha Tanzania katika Michezo ya Olimpiki na kuleta medali na michezo mbalimbali ya kimataifa.

Laura amesema Shule ya Msingi ya Steiner Waldorf inawawezesha watoto kujifunza shughuli za kijamii na mazingira, kukuza ubunifu na fikra huru na kuongeza michezo ya vikwazo ni fursa mpya.

“Shule yetu ya sekondari inahakikisha wanafunzi wetu wa msingi wanaendelea na masomo yao katika madarasa madogo na walimu waliofunzwa katika mazingira ya kuunga mkono na maendeleo yao na kujenga jamii bora,” ameongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles