Na WINFRIDA MTOI- DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Mbao, Fred Minziro, ameweka wazi maeneo aliyoanza kuyasuka ili kuinusuru timu hiyo na janga la kushuka daraja.
Minziro alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Mbao wiki iliyopita akichukua nafasi ya Hemedi Suleiman ‘Morocco’, aliachana na kikosi hicho tangu mwaka jana.
Alizungumza na MTANZANIA jana kabla ya mchezo wao na Coastal Union, Minziro alisema kwa siku alizofanya mazoezi na timu hiyo alijaribu kuangalia zaidi maeneo manne.
Minziro alitaja maeneo hayo kuwa ni safu ya ushambuliaji, kumiliki mpira, ulinzi na kiungo.
“Ni ngumu kueleza kwa sasa kuwa timu itabaki au itashuka kwa sababu bado tuna mechi zimebaki, lakini kikubwa nimejaribu kuanza na maeneo ya msingi amabyo yanaweza kutupa matokeo mazuri.
Ukiangalia nafasi tuliyopo, kinachotakiwa ni kushinda mechi zilizobaki ili kujitoa chini, naamini tunaweza kufanikiwa, nitachokata ni timu kucheza mpira,” alisema Minziro.