28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Silaa aweka mikakati ya kuboresha sekta ya habari kupitia ushirikiano na wanahabari

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, ameeleza mikakati ya kuboresha sekta ya habari kupitia ushirikiano wa karibu na wanahabari, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akizungumza leo Novemba 18, 2024 jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wadau wa habari, Waziri Silaa alisisitiza dhamira ya serikali kufanya marekebisho ya sera na sheria ili kuendana na mahitaji ya kisasa. Alibainisha kuwa sekta ya habari ni mhimili wa maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kiusalama, huku ikiwa nguzo ya uwazi na uwajibikaji wa serikali.

Silaa alifafanua kuwa serikali tayari imepiga hatua kwa kuondoa adhabu za kijinai kwa makosa ya kashfa, na hivyo kuimarisha uhuru wa wanahabari na maoni. Aliahidi kutembelea wadau mbalimbali wa habari ili kubadilishana mawazo na kutafuta njia za kuimarisha sekta hiyo.

Akiwapongeza wanahabari kwa mchango wao katika kufanikisha mawasiliano ya miradi ya maendeleo, alitoa wito wa kuendelea kufuata maadili na sheria, hususan katika kipindi cha uchaguzi. Alisisitiza kuwa historia ya vyombo vya habari nchini ni msingi wa umoja wa kitaifa, akitoa mfano wa mchango wa vyombo hivyo katika harakati za uhuru.

Waziri Silaa amedhamiria kuimarisha ushirikiano na wanahabari ili kuhakikisha sekta hiyo inatoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles