28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

THDRC yasisitiza maboresho ya usimamizi wa majengo na majanga

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THDRC) umehimiza serikali kuweka mifumo madhubuti ya usimamizi na ufuatiliaji wa uhai wa majengo, hasa ya umma na biashara, ili kuepusha athari kama zilizotokea kwenye tukio la kuanguka kwa jengo Kariakoo.

Akizungumza Novemba 18, 2024, jijini Dar es Salaam, Mratibu wa THDRC, Wakili Onesmo Ole Ngurumwa, alisema mamlaka za serikali zinapaswa kuimarisha ufuatiliaji wa vibali na ukaguzi wa majengo. Pia, alihimiza maboresho ya sheria inayosimamia majanga ili kuunda kamati za kudumu za kusimamia na kuzuia majanga kwa muda mrefu badala ya kuunda kamati baada ya matukio.

“Majanga ni suala endelevu. Tunapendekeza kamati ya kudumu ya majanga ambayo itaendelea kutoa elimu kwa wananchi na kufuatilia hatua za kuzuia majanga,” alisema Ole Ngurumwa.

Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza kampeni Novemba 20, alisema mtandao huo umehimiza kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki, huku serikali zikihimizwa kuweka mifumo bora ya usimamizi wa uchaguzi.

Ole Ngurumwa pia alizungumzia maendeleo ya Tarafa ya Ngorongo, akieleza kuwa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan yameanza kutekelezwa kwa kuweka kambi za tathmini ya mahitaji, zikiwemo fedha kwa ukarabati wa shule, zahanati, barabara, na huduma za msingi. Alifichua kuwa tarafa hiyo inahitaji shilingi bilioni 2 kwa ajili ya maendeleo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles